Tetesi za Mastaa Ulaya: Man United Yajitoa Kushindania Saini ya Harry Kane

Manchester United imesema haitashindania saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa England na Tottenham Hotspur Harry Kane, 29, kutokana na kiwango kikubwa cha fedha ambacho Spurs wanakihitaji.

Mauricio Pochettino hana wakala kwa wakati huu ambapo anakaribia kuichukua Chelsea kama kocha mpya kuchukua nafasi ya Graham Potter.

Kocha wa Hispania David Raya na mshambuliaji wa England Ivan Toney, wote wakiwa na miaka 27 wakicheza Brentford wanatajwa kuwa kwenye rada za Chelsea.

Liverpool hawako tayari kutumia kiwango kikubwa cha fedha kwenye kumnunua kiungo wa Inter Milan Nicolo Barella, 26, ingawa haijajitoa kwenye nia ya kumsajili Jude Bellingham wa Borussia Dortmund.

Author: Asifiwe Mbembela