United Yatinga Fainali FA, Yaichapa Brighton

Manchester United imefuzu kucheza fainali ya Kombe la FA baada ya kuifunga kwa penati Brighton Hove Albino 7-6 baada ya sare tasa kwenye dakika 90 pamoja na dakika 30 za muda wa ziada.

Licha ya kuwa na kiwango kizuri kwa muda wote wa dakika 90 ongeza nyongeza, Solly March ameinyima nafasi timu yake kushinda taji la kwanza la Kombe la FA kwani penati yake ilipaa kabla ya Victor Lindelof kufunga na kufanya Man kufuzu fainali.

Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kufuzu kucheza fainali mbili ndani ya msimu mmoja baada ya kushinda mapema Kombe la Carabao mwezi Februari.

Fainali itapigwa Juni 3 kwenye dimba la Wembley ambapo nusu fainali zote mbili zimechezwa hapo.

Author: Bruce Amani