Tetesi za Mastaa Ulaya: Chelsea Imefanya Mawasiliano na Mourinho

Chelsea imefanya mawasiliano ya kocha wa zamani wa timu hiyo Jose Mourinho ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha AS Roma ya Italia kwa ajili ya kuona uwezekano wa kumpata kurithi mikoba ya Graham Potter darajani.

Mourinho mkononi mwake pia anayo ofa ya kuinoa timu ya taifa ya Saudi Arabia ambayo ipo tayari kumlipa Euro milioni 120.

Inter Milan wanakusudia kumtia kitanzi mlinzi wake raia wa Italia Alessandro Bastoni, 23, kwa kumpa mkataba mpya ili kumuweka kando na tetesi za kuhusishwa kujiunga na Manchester City.

Barcelona na Bayern Munich wanaweza kuipiku Manchester United katika kuipata saini ya beki wa kulia wa Uholanzi na Bayer Leverkusen Jeremie Frimpong, 22.

Author: Bruce Amani