Tetesi za Mastaa Ulaya: Mount Aingia Rada za Arsenal

Arsenal wanaendelea kumfuatilia kiungo mshambuliaji wa Chelsea na England Mason Mount, 24, ambaye nafasi yake The Blues imekuwa finyu kila wakati hata chini ya Frank Lampard.

Paris St-Germain wanaandaa dau la pauni milioni 133 kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria na Napoli Victor Osimhen, 24, ambaye amekuwa kwenye ubora mkubwa.

Mauricio Pochettino anaongoza kinyang’anyiro cha kuchukua nafasi ya kuinoa Chelsea ambayo haina kocha baada ya Graham Potter kufutwa kazi.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Roberto Firmino, 31, amekubali mkataba wa kujiunga na Barcelona baada ya kandarasi ya sasa kumalizika Liverpool.

Author: Bruce Amani