Borrusia Dortmund yaipa Manchester United siku 6 kukamilisha usajili wa Jadon Sancho

Klabu ya Borussia Dortmund imeipa klabu ya Manchester United siku 6 kukamilisha uhamisho wa staa wa Kiingereza Jadon Sncho, 20. Tayari klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ujerumani imeshawaambia United kuwa inataka pauni milioni 100 ili kumpa staa huyo.

Hakuna makubaliano yoyote ambayo yamefikiwa kwenye masuala ya pesa ingawa mambo binafsi ya mchezaji na klabu inaonekana kutokuwa taabu. Dortmund wamewapa Manchester United siku ya mwisho ya kuhakikisha inakamilisha usajili kwani imesema haihitaji usumbufu pindi wakianza maandalizi ya msimu ujao 2020/21.

Msimu mpya wa Ujerumani umepangawa kuanza Sept 18 ambapo tarehe ya mwisho za usajili imepangwa kuwa Oct 5. Sancho amekuwa ndani ya uzi wa Borrusia Dortmund kwa miaka mitatu tangu aliposajiliwa na klabu hiyo akitokea kwa Mabwenyenye wa Jiji la Manchester, Manchester City Agosti 2017 kwa dau la pauni milioni 10.

Author: Bruce Amani