Chelsea au Madrid? Hazard njia panda

Eden Hazard anasema bado yupo njia panda, ama kusaini mkataba mpya Stamford Bridge au kwenda kwenye klabu ya ndoto yake “Real Madrid”

Mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji bado ana mkataba wa miaka miwili na Chelsea, lakini amekuwa akihusishwa na minong’ono kwamba anataka kujiunga na Real Madrid katika uhamisho wa majira yajayo ya joto.

Hazard tayari amezifumania nyavu mara saba katika Premier Legue msimu huu.

“Sitaki kusema ndio, ninasaini mkataba mpya, halafu baadae sisaini,” alisema Hazard mwenye miaka 27 kwa waandishi wa habari.

“Ninataka kilicho bora kwangu, lakini pia ninataka kilicho bora kwa klabu kwa sababu ilinipatia kila kitu”. Kwa hiyo nitaangalia. Mara nyingine kichwani mwangu, huwa naamka asubuhi nawaza ninataka kuondoka, na mara nyingine nafikiria ninataka kubaki, ni maamuzi magumu. Ni mustakabali wangu.” Alisema Hazard.

Mshambuliaji huyo anaamini bado anahitaji kwenda mahali pengine kabla ya kuachana na soka, huku akiielezea Real Madrid kuwa ni “klabu bora zaidi duniani”

“”Real Madrid ni klabu boa zaidi duniani. Sitaki kudanganya. Ni ndoto yangu tangu utotoni, Nilikuwa naota kuhusu hii klabu”.

Author: Bruce Amani

ChelseaHazardReal madrid