Gor wakabidhiwa rasmi Kombe la KPL

Gor Mahia walinyanyua Kombe la Ligi Kuu ya Kandanda nchini Kenya kwa mara ya 17 katika sherehe iliyofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Moi mjini Kisumu.

Hata hivyo vijana hao wa kocha Dylan Kerr walilazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili na Mathare United licha ya kuwa wao ndio walikuwa kifua mbele 2-0 kupitia mabao ya Jaques Tuyisenge na Humphrey Mieno. Mathare walisawazisha kupitia Cliff Nyakeya na Omulanga.

Nahodha Harun Shakava alitwaa Kombe baada ya kukabidhiwa na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga ambaye alikuwa mgeni wa heshima.

Mechi ya leo ilikuwa ya nne mfululizo kwa mabingwa hao kupoteza kitu ambacho nahodha Shakava alisema kinasikitisha sana. Gor wamebaki na mechi mbili kabla ya kukamilisha msimu dhidi ya Zoo Kericho na Tusker FC

Gor walifanya msafara wa kwenye barabara za mji wa Kisumu kuwaonyesha mashabiki Kombe na kusherehekea ubingwa wao.

Author: Bruce Amani

Gor MahiaTusker