Inter Yaitandika Benfica

Romelu Lukaku amefunga goli moja kwenye ushindi wa 2 – 0 ambao wameupata Inter Milan dhidi ya Benfica katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali uliochezwa Lisbon.

Nicolo Barella alianza kuipa uongozi Inter akifunga kwa kichwa kabla ya dakika za lala salama Lukaku ambaye mchezo wa wikiendi alionyeshwa kadi nyekundu kutokana na aina yake ya ushangiliaji.

Benfica wakiwa mbele ya mashabiki wao walishindwa kuifungua safu ya ulinzi na Inter ambayo imekuwa uchochoro kwenye Serie A msimu huu.

Mlinda mlango wa Inter Andre Onana akizungumzia matokeo hayo amesem bado hawajafuzu na hawawezi kujiona umefuzu hata kabla ya kucheza.

Author: Bruce Amani