Milan Yafuzu Nusu Fainali Mbele ya Napoli

AC Milan imetinga kibabe nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia kuibuka na ushindi wa jumla ya bao 2-1 katika michuano ya robo fainali mkondo wa kwanza na ugenini baada ya leo kutoa sare ya bao 1-1 na Napoli.

Milan walianza San Siro kwa kuvuna ushindi mwembamba wa goli moja kwa sifuri kabla ya leo kutoa sare ya 1-1 kwenye mechi ambayo wachezaji wa timu hizo wawili walikosa penati kwa nyakati tofauti.

Kwa Milan inakuwa mara ya kwanza wanafuzu nusu fainali tangia mwaka 2007 ambapo sasa watacheza na Benfica ama Inter Milan ambayo inaongoza bao 2-0 mabao waliyoyapata kwenye mechi ya kwanza.

Mabao kwenye mechi hiyo yakafungwa na Olivier Giroud kwa AC Milan kabla ya bao la dakika za nyongeza za ungwe ya pili likiwekwa kimiani na Victor Osimhen.

Author: Bruce Amani