Lukaku Ashinda kesi ya kufungiwa Mechi Moja

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji Romelu Lukaku ‘Big Rom’ ameshinda adhabu ya kufungiwa mechi moja kufuatia kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi kutokana na aina yake ya ushangiliaji.

Lukaku alionyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kufunga penati dakika za mwishoni kwenye mechi ya nusu fainali dhidi ya Juventus. Baada ya kufunga alichukua kidole chake na kuziba mdomo huku mkono mwingine ulionyesha ishara ya “salute” kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa ni utovu wa nidhamu.

Kutokana na kadi hiyo, Lukaku mchezaji wa zamani wa Everton, Chelsea na Manchester United alisema kuwa alifanya vile ili kupinga ubaguzi ambao alikuwa anaupata kabla, wakati na hata baada ya mchezo.

Baada ya wawakilishi wa mchezo huyo kupinga adhabu ya kufungiwa mechi moja katika mahakama ya rufaa FIGC hatimaye ameshinda na Lukaku ameelezea kitendo hicho kama ni ishara na matamanio ya kupigana vuta dhidi ya ubaguzi.

 

Author: Bruce Amani