Man City Yaanza Kwa Ushindi Mbele ya Bayern Munich

Manchester City wameanza vyema katika kuwania nafasi ya kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia kuibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Bayern Munich mchezo wa robo fainali uliochezwa uwanja wa Etihad Jijini Manchester.

City ambayo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, magoli yake yamefungwa na Rodri dakika ya 27 kwa shuti kali, Bernardo Silva dakika ya 70 na Erling Haaland dakika ya 76.

Akicheza dhidi ya timu yake ya zamani, kocha Pep Guardiola aliweza kuizidi Bayern kwenye nyanja nyingi uwanjani kabla kupata bao hizo huku mshambuliaji wake Erling Braut Haaland akiendelea kutunza historia kwenye vitabu mbalimbali duniani.

Kwingineko, Inter Milan imeshinda bao 2-0 dhidi ya Benfica mabao ya Nicolo Barella na Romelu Lukaku.

Mechi za marudiano zitachezwa Aprili 19.

Author: Bruce Amani