Lukaku, Cuadrado Waonyeshwa Kadi Nyekundu

Mabingwa watetezi wa Kombe la Coppa Italia Inter Milan wametoa sare ya bao 1-1 na Juventus katika mchezo wa nusu fainali ya mashindano hayo uliochezwa Jumatano usiku dimba la Allianz.

Katika mchezo huo, Juan Cuadrado alifunga bao la uongozi kabla ya Romelu Lukaku aliyetokea benchi dakika ya 69 na kuingia na kusawazisha bao la mkwaju wa penati dakika ya 95 kabla ya huo huo muda kuonyeshwa kadi nyekundu.

Lukaku ambaye amefunga mabao matano kwenye mechi 20, alitupwa nje kutokana na aina yake ya ushangiliaji mbele ya mashabiki wa timu yake.

Nahodha wa Inter ambaye ni kipa Samir Handanovic na Cuadrado walionyeshwa kadi nyekundu baada ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi.

Cremonese itacheza Leo Jumatano na Fiorentina katika nusu fainali ya pili.

Author: Asifiwe Mbembela