Napoli Yaichapa Sassuolo, Osimhen a endelea kupaa

Vinara wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A Napoli wameendelea kuthibitisha ubora wao msimu huu kwa kutanua mwanya kileleni kwa tofauti ya pointi 18 dhidi ya timu iliyo nafasi ya pili Inter Milan baada ya ushindi mjarabu wa bao 2-0 dhidi ya Sassuolo ugenini.

Mabao ya Napoli kwenye mechi hiyo yamefungwa na Khvicha Kvaratskhelia kunako dakika ya 12 ya mchezo akimalizia kwa shuti dogo kiasi baada ya mpira wa kona.

Mshambuliaji hatari kwa hivi sasa wa timu hiyo Victor Osimhen alifunga bao la pili kwa Napoli dakika 33 tangia kuanza kwa mchezo na kufanya matokeo kuwa 2-0.

Bao moja ambalo alilifunga Osimhen kwenye mchezo huo linamfanya kufunga kwenye mechi saba mfululizo za Serie A na kuna kila dalili kuwa anaweza kuisaidia Napoli kushinda taji la tatu la Ligi Kuu Italia baada ya kutwaa mara ya kwanza mwaka 1989/90.

Author: Bruce Amani