Juventus Yapokonywa Pointi 15, Yashushwa Mpaka Nafasi ya 11

Miamba ya soka la Italia Serie A Juventus imepokonywa alama 15 na Shirikisho la Kandanda nchini Italia FIGC kufuatia uchunguzi uliofanywa kubaini makosa katika usajili wa klabu hiyo kwa misimu kadhaa iliyopita.

Shirikisho hilo limesema kuwa Juve walikuwa wanaongopa kwenye daftari la usajili na kuonekana kuna uwiano wa mauzo na maingizo ya wachezaji kumbe haikuwa hivyo.

Kabla ya kupokonywa alama 15, Juventus walikuwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Italia lakini sasa wanashuka mpaka nafasi ya 11.

Pamoja na kupokonywa alama hizo, Juventus wamekana kuhusika na tuhuma hizo. Jumapili watakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Atalanta, Serie A.

Author: Bruce Amani