Juventus Yabanwa 3-3 na Atalanta

Juventus imefanikiwa kuvuna alama moja nyumbani dhidi ya Atalanta katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A uliomalizika kwa sare ya bao 3-3.

Atalanta ikiwa moja ya timu zenye uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi za magoli ilichukua uongozi kupitia kwa Ademola Lookman lakini Juventus miamba ya soka la Italia waliweza kurudi kibabe na kuongoza kwa mabao ya Angel di Maria na Arkadiusz Milik.

Joakim Maehle wa Atalanta alisawazisha kisha nyota wa zamani wa Everton Lookman akafunga bao la pili kwake na la tatu katika mchezo huo.

Nusura ya Juve ilikuwa ni beki Danilo ambaye alifunga bao la tatu na kufanya mchezo huo kuwa sare ya 3-3.

Matokeo hayo yanaifanya Atalanta kushika nafasi ya tano wakati Juventus wakikwea mpaka nafasi ya tisa.

Author: Bruce Amani