Napoli Yaichapa 2-1 Atalanta

Napoli wamerudi kwenye njia za ushindi baada ya wiki iliyopita kukutana na kipigo kutoka kwa Lazio, leo wameichapa Atalanta bao 2-0 mchezo uliochezwa nyumbani kwa Napoli.

Mabao ya kikosi cha kocha Luciano Spalletti yamefungwa na Khvicha Kvaratskhelia pamoja na lile la Amir Rrahmani ambapo mshambuliaji wa timu hiyo Victor Osimhen alisaidia upatikanaji wa goli moja.

Matokeo hayo yanaifanya Napoli kufikisha mechi 22 za ushindi kwenye Ligi Kuu ya Serie A wakiwa kileleni kwa tofauti ya pointi 18 mechi 12 zikiwa zimesalia.

Author: Bruce Amani