Juve yaizamisha Napoli

Mario Mandzukic alifunga mabao mawili wakati Juventus ilizoka nyuma na kuizaba Napoli mabao matatu kwa moja na kutanua pengo la pointi sita dhidi ya timu hiyo ya Carlo Ancelotti kileleni mwa ligi.

Cristiano Ronaldo alikuwa na mchango mkubwa katika mabao yote matatu wakati timu hiyo ya Massimiliano Allegri ilihakikisha kuwa inakusanya pointi 21 baada ya kucheza mechi saba. Napoli wana pointi 15, baada ya kupewa kichapo cha pili msimu huu.

Awali, Roma iliwashinda watani wao wakali Lazio mabao matatu kwa moja na kuendelea kujiimarisha baada ya mwanzo mbaya wa msimu. Ushindi huo umeiweka Roma katika nafasi ya sita na pointi 11 nyuma ya Lazio katika nafasi ya tano ikiwa na pointi 12 baada ya mechi saba.

Inter Mian ilipata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Cagliari uwanjani San Siro. Vijana hao wa kocha Luciano Spalletti sasa wako katika nafasi ya nne na pointi 13 mbele ya Lazio na Roma.

Author: Bruce Amani

AllegriAncelottiJuventusNapoliRonaldo