Azam yabanwa na Mbeya City

Azam FC imeshindwa kutumia faida ya kuwa nyumbani mbele ya mashabiki wake na kuibuka na ushindi katika mechi dhidi ya Mbeya City ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo uliopigwa dimba la Azam Complex Jijini Dar es Salaam Leo Jumamosi Disemba 18 na mtanange huo umemalizika kwa sare ya goli 2-2.

Mabao katika mchezo huo yamefungwa na Bruce Kangwa na Never Tigere kwa upande wa Azam Fc na yale mabao ya Mbeya City yamefungwa na Juma Luizio dakika ya 28 na Richardson Ng’odya dakika ya 65.

Azam FC inafikisha pointi 12 katika nafasi ya saba na Mbeya City sasa ina pointi 15 na kupanda nafasi ya tatu baada ya timu zote kucheza mechi tisa sasa.

Author: Asifiwe Mbembela