Borrusia Dortmund yaichapa Club Brugge na kuongoza kundi F

Erling Haaland ameendelea kuwa na rekodi za hatari akiwa karibu ya eneo la 18 la mpinzani baada ya Jumatano kutupia bao mbili wakati Borrusia Dortmund ikiiadhibu Club Brugge goli 3-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Uefa uliopigwa nchini Ubeligiji.

Haaland, 20, alitupia goli zote mbili kipindi cha kwanza sawa na mchezaji mwenza Thorgan Hazard ambaye alifunga goli la kwanza kwa klabu hiyo shiriki Ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani.

Tangu alipojiunga na Dortmund mwishoni mwa mwezi Januari 2020, Haaland amekuwa habari nyingine, ambapo amefunga goli 26 katika mechi 28 pekee mashindano yote. Katika Ligi ya Mabingwa, amefunga goli 14 mechi 11 zikiwa ni mechi chache zaidi kwa mchezaji kufikisha idadi hiyo ya mabao.

Dortmund wanaongoza kundi F alama sita tofauti ya alama moja na Lazio walio nafasi ya pili katika kundi hilo.

Author: Bruce Amani