Chelsea, Porto kumalizana Hispania Ligi ya Mabingwa Ulaya

Mechi mbili za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ya Chelsea dhidi ya FC Porto itachezwa katika dimba la Seville nchini Hispania kutokana na vizuizi vya Covid-19.

Mitanange hiyo miwili itachezwa katika dimba la Ramon Sanchez-Pizjuan, uwanja ambao hutumiwa na klabu ya Sevilla ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Hispania La Liga.

Mkondo wa kwanza utapigwa Aprili 7 na mkondo wa pili utakuwa Aprili 13.

Awali, mchezo wa raundi ya kwanza wa hatua ya 16 bora wa Chelsea dhidi ya Atletico Madrid ulichezwa Bucharest kutokana na sababu kama hizo.

Author: Asifiwe Mbembela