Chelsea yaishushia kibano Malmo Ligi ya Mabingwa

Chelsea imerudisha nguvu ya kuwania taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuitandika Malmo goli 4-0 katika mchezo uliopigwa dimba la Stamford Bridge huku ikishuhudiwa nyota Romelu Lukaku na Timo Werner wakiumia na kulazimika kutolewa kwa nyakati tofauti.

Mabingwa watetezi hao walianza kupata goli kupitia kwa beki wa kati Andres Christensen ambaye ni goli la kwanza kwenye mechi 137, kabla ya kiungo mkabaji Jorginho kufungwa mkwaju wa penati baada ya Bolingoli Romelu Lukaku kufanyiwa faulo na Lasse Nielsen.

Licha ya Timo Werner kutolewa lakini bado Chelsea iliendelea kushambulia ambapo Callum Hudson Odoi alitengeneza goli kwa Kai Havertz kabla ya Jorginho kurudi tena na kufunga goli la penati, akiwa mchezaji wa kwanza wa Chelsea kufunga goli la penati kwa makipa wawili tofauti tangia mwaka 1999, kufuatia Malmo kufanya mabadiliko ya makipa mapumziko

Author: Bruce Amani