Hazard akwamisha mpira nyavuni wakati Real Madrid wakishinda mbele ya Inter Milan

Matumaini ya Inter Milan ya kufuzu kuingia hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa yameanza kuingia gizani kufuatia kukutana na kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa Real Madrid katika dimba la San Siro Jana Jumatano.

Kiungo mkabaji wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich Arturo Vidal alitimuliwa uwanjani kwa kuonyeshwa kadi mbili za njano na refarii wa England Anthony Taylor jambo lililoleta utofauti mkubwa baina ya timu hizo.

Kisha Eden Hazard akatupia bao la kwanza kwa Madrid kwa njia ya penati na kisha goli la kujifunga la beki wa zamani wa Borrusia Dortmund na Real Madrid Achraf Hakimi.

Antonio Conte na kikosi chake wamepata alama mbili kwenye mechi nne walizocheza huku mbili pekee zikiwa zimesalia katika kundi B.

Ushindi unaifanya Madrid kushika nafasi ya pili alama moja nyuma ya Borrusia Monchengladbach. Kwingineko, Gladbach walishinda bao 4-0 dhidi ya a Shakhtar Donetsk wakifunga goli tatu ungwe ya kwanza na kumalizia sherehe kwa goli moja ungwe ya pili.

Author: Bruce Amani