Jukwaa tayari kwa kivumbi cha Simba na Yanga

Mtanange wa watani wa Jadi nchini Tanzania mabingwa watetezi Simba na mabingwa wa zamani Yanga FC unaendelea kusubiriwa kwa hamu.

Mechi hii itakazopigwa Jumapili 30.09 hufahamaika kama Dar es salaam au Kariakoo Derby.

Kuelekea mchuano huo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya soka nchini humo, mashabiki wameanza kutupiana maneno kuhusu mshindi wa Jumapili.

Simba inakwenda katika mechi hii ikiwa imefanya usajili wa Mabilioni ya fedha za nchi hiyo huku Yanga ikikabiliwa na changamoto za kifedha.

Timu hizi mbili zinakwenda katika mechi hii, zikiwa haziongozi msimamo wa ligi ambao kwa sasa unashikiliwa na Mtibwa Sugar na Mbao FC.

Yanga FC, ni ya tatu kwa alama 12 baada ya mechi nne, huku Simba ikiwa katika nafasi ya tano kwa alama 10 baada ya mechi tano, nyuma ya Azam FC.

Author: Bruce Amani