Kocha wa Real Madrid Zidane akubali lawama za kipigo cha Shakhtar Donetsk

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema lawama za kipigo cha goli 3-2 dhidi ya Shakhtar Donetsk katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi zinapaswa zimuendee yeye na sio wachezaji.

Jana Jumatano, Madrid wakiwa dimba la nyumbani walijikuta wakiwa nyuma kwa goli mbili za haraka za Donetsk kabla ya kuongezwa bao la tatu kwa mabingwa hao mara 13 wa Ligi ya mabingwa Ulaya.

Kitu cha ajabu, Shakhtar Donetsk ya nchini Ukraine ilisafiri kwenda kuwakabili Madrid bila ya wachezaji 13 wa kikosi cha kwanza kutokana na kuwa na dalili za Covid-19 na kulazimika kuwajumuisha wachezaji wa timu za vijana lakini haikuwazuia kutoa kichapo hicho cha fedheha kwa kocha Zidane na timu kwa ujumla.

Bao la Luka Modric na Vinicius Junior kipindi cha pili yameipa auheni Madrid kufungwa nyumbani Bernabeu 3-0. Akizungumza baada ya mchezo amesema yeye (Zidane) ndiye anapaswa kulaumiwa kutokana na kichapo hicho.

Author: Asifiwe Mbembela