Liverpool yaishushia Atalanta kipigo cha mbwa koko

Kikosi cha Atalanta kimekutana na mateso ya kutosha kutoka kwa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Liverpool kwa mwaka 2018 baada ya kupewa kichapo cha goli 5-0 kwenye mchezo uliopigwa Jana Jumanne. Mateso hayo kwa kiasi kikubwa yamechagizwa na fomu aliyokuwa nayo winga Diogo Jota akifunga bao tatu hat-trick katika mchezo huo, mabao mengine yakifungwa na Sadio Mane na Mohammed Salah.

Mechi hiyo inakuwa ya tatu kwa kocha Jurgen Klopp kupata matokeo chanya katika kundi D bila kuruhusu wavu wake kuguswa, ushindi mmoja pekee umesalia kujikatia tiketi ya kucheza hatua ya mtoano, 16 bora.

Swali kubwa ambalo Klopp atakuwa nalo kichwaani mwake ni juu ya kuendelea kumtumia mshambuliaji wake Roberto Firmino kwani katika mechi hiyo aliwekwa bechi na kumtumia Diogo Jota nyota wa zamani wa Wolverhampton Wanderes ambaye alikopeshwa imani amelipa fadhila

Katika kundi hilo, Ajax wamepata ushindi wa kwanza kwa kuifunga goli 2-1 Midtjylland, matokeo yanayoifanya Midtjlland kubaki mkiani kwenye msimamo wa kundi hilo.

Author: Asifiwe Mbembela