Bilionea wa Simba Mo Dewji atekwa Tanzania

Mwanachama maarufu wa Simba SC na bilionea kijana wa Simba, Mohamed Dewji ametekwa na watu wasiojulikana asubuhi ya leo jijini Dar-es-Salaam.

Akiongea na kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM asubuhi ya leo Oktoba 11- 2018 kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni ACP Jumanne Muliro amethibitisha taarifa hizo na kusema jeshi la polisi linafanya uchunguzi juu ya tukio hilo na litatoa tarifa hapo baadaye

Taarifa kutoka katika eneola tukio zinasema kuwa Mohamed Dewji maarufu kama “Mo” ametekwa na watu walio na silaha za moto wakati akiingia gym ya Collesium jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo.

Taarifa zaidi zitafuata……..

Author: Master Tindwa