Simba, Yanga zatoshana nguvu

Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ulianza kufurika tangu saa za mchana, tayari kwa mtanange ambao huvutia hisia nyingi sana sio tu nchini Tanzania bali Afrika Mashariki. Mchuano wa watani wa jadi kati ya vigogo wa ligi kuu ya kandanda ya Tanzania bara Simba SC na Yanga.

Na baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa, hakuna aliyeona lango la mwenzake na hivyo ikabidi wagawane pointi tatu. Simba kupitia washambuliaji wake Emmanuel Okwi na Meddy Kagere walipoteza nafasi kadhaa za wazi wakati pia Yanga wakionekana kutojua ziliko nyavu za Wekundu wa Msimbazi.

…….maelezo zaidi yatafuata…

Author: Bruce Amani

SimbaYanga