Brazil yahifadhi ubingwa wa Olimpiki kwa kuifunga Hispania 2-1

Timu ya taifa ya Brazil imeibuka na ushindi muhimu dhidi ya taifa la Hispania kwa ushindi wa goli 2-1 katika muda wa ziada kwenye mashindano ya Olimpiki Tokyo 2020 na kufanikiwa kutetea taji lake.

Mchezaji wa akiba Malcom aliingia na kufunga goli bora akitumia vyema makosa ya mlinzi kunako dakika ya 108, bao ambalo limewapa medali.

Itakumbukwa miaka mitano ijayo, mshambuliaji wa Brazil Neymar Jr alifunga goli la ushindi kwa njia ya penati ya mwisho mbele ya Ujerumani katika uwanja wa nyumbani Brazil.

Bao la Mikel Oyarzabal wa Hispania lilifuta goli la Matheus Cunha aliyefunga goli awali kwenye muda wa kawaida, muda huo wakati Richarlison akiwa amekosa penati

Author: Bruce Amani