IOC yapinga Kombe la Dunia kufanyika baada ya miaka miwili

Kamati ya Mashindano ya Kimataifa wa Olympiki (IOC) inaamini kuwa mpango wa Shirikisho la Kandanda Duniani Fifa wa kuandaa fainali za Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili unatishia ubora wa michezo mengine na usawa wa kijinsia.

Inaaminika kuwa kufanyika kwa Kombe la Dunia baada ya miaka miwili kutaleta msigano wa michezo mingine hasa michezo ya Olympiki pamoja na mashindano makubwa ya Wanawake yaliyoko kwenye kalenda.

IOC kupitia taarifa yake ilisema kuwa migogoro na matukio mengine ya kimichezo inaweza kushusha ukuaji wake sawa na kushusha usambaaji wa michezo maeneo mengine.

Taarifa hiyo pia imeongeza kuwa michezo ya wanaume itaongeza changamoto kwa michezo upande wa Wanawake jambo ambalo siyo nzuri.

Siku za karibuni kumekuwa na mjadala wa kupunguza muda wa kufanyika kwa Kombe la Dunia kutoka miaka minne iliyopo sasa mpaka miwili, sababu kubwa ya mpango huo ni kuwafanya wachezaji kushiriki michuano hiyo mikubwa duniani angalau mara nyingi na masuala ya kifedha.

Author: Bruce Amani