Yanga yashinda mechi ya mwisho ya Kombe la Mapinduzi

Klabu ya Yanga imemaliza mechi yao ya mwisho ya hatua ya makundi katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kuichapa Jamhuri kwa mabao 3-1 katika mtanange uliofanyika Dimba la Amaan Visiwani Zanzibar.

 

Katika mchezo huo kila timu ilionyesha kiwango kizuri kutokana na presha ndogo ya mchezo kwani timu zote zilikuwa zinakamilisha ratiba ya michuano hiyo tu kwani zote zimeondoshwa.

 

Magoli yote 4 yalipatikana kipindi cha kwanza huku magoli ya Yanga yakifungwa na Faraji Kilaza, Shaaban Mohamed na Pius Buswita.

 

Kinda Gustafa Saimon wa Yanga mbali na kuondoshwa kwa timu yake bado ameonyesha kiwango bora sana katika michuano hiyo. Goli la Jamhuri lilifungwa kunako dakika ya 3 na Hajji Ramadan baada ya Kazi kubwa Husse Rajab. 

 

Yanga inandoka Zanzibar baada ya kujikusanyia alama 6 ikiwa imeshinda michezo miwili na kufungwa miwili huku Azam Fc na Malindi zikisonga mbele fatica kundi B.

Author: Bruce Amani