Cavani kuongezewa muda wa kuichezea Manchester United

Kocha Mkuu wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa wako kwenye mchakato wa kumuongezea muda wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho mshambuliaji Edison Cavani. Mshambuliaji huyo raia wa Uruguayi mwenye umri wa miaka 33 alijiunga na Manchester United kwa mkataba wa mwaka mmoja mwezi Octoba kukiwa na kipengele cha kuongeza muda zaidi.

Cavani ameanza mechi moja pekee kati ya nane za EPL ambapo amefunga goli tatu na kusaidia lingine moja alilompa Bruno Fernandes siku ya Jumamosi dhidi ya Leicester City..

Solskjaer alisema anategemea Cavani atakubali mkataba mpya wa kuendelea kubakia hapa. Meneja huyo wa United alisema nyota huyo ana msaada kwenye timu zaidi ya kutokea bechi kwani amekuwa akitoa uzoefu wake kwa wachezaji vijana kama Mason Greenwood.

Author: Asifiwe Mbembela