Lamine afunga ndoa ya kudumu Jangwani Yanga

Yanga imethibitisha kuingia kwenye mkataba mpya na beki kitasa wa timu hiyo raia wa Ghana Lamine Moro ambaye awali kulikuwa na taarifa kuwa kandarasi yake inaelekea tamati mwishoni mwa msimu huu.
Yanga SC kupitia kwa Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, Eng. Hersi Said, wamethibitisha kuwa Beki wao wa kimataifa  Mghana Lamine Moro ameongeza mkataba wa kuichezea hadi mwaka 2023.
Lamine, hivi karibuni iLiripotiwa kuwa mkataba wake unakaribia kufika ukingoni jambo ambalo limewafanya mabosi wake kumpa dili jipya kutokana na uwezo wake kuwa ndani ya uwanja.
Lamine amesema: “Ni kweli nimeona vyema kuongeza mkataba, kwanza itanipa muda zaidi wa kutekeleza majukumu yangu.”
Beki huyo kisiki alijiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Bidcom ya Zambia mkataba ambao unamalizika mwishoni mwa msimu ujao. Lamine ataendelea kubaki mitaa ya Jangwani  hadi Julai 2023.
Ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu huu 2020/21 akiwa amecheza mechi tatu na amefunga mabao mawili.

Author: Asifiwe Mbembela