Nigeria Yaichapa 10-0 Sao Tome and Principle Kufuzu Afcon 2023

Timu ya taifa ya Nigeria imetoa kichapo kizito kwa kibonde Sao Tome and Principle cha bao 10-0 mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika Afcon 2023 hatua ya makundi Kundi A.

Kwenye ushindi huo mzito ambao unakuwa kama kuwafuta machozi Super Eagles baada ya kupoteza nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia Qatar umepatikana kupitia wachezaji wengi lakini kiboko ni Victor Osimhen ambaye amefunga mabao manne.

Unakuwa ushindi mkubwa nje na mechi za nyumbani kwa Nigeria ambao mara ya mwisho kuibuka na idadi ya magoli hayo ilikuwa mwaka 1959 waliposhinda bao 10-1 kwa Benin.

Wachezaji wengine ambao wamefunga magoli ni strika wa Watford Emmanuel Dennis, wa Leicester City Ademola Lookman, na Jose Peseiro.

Nigeria inakuwa timu ya tano kubwa kuanza kwa kushinda kwenye mechi mbili za awali hatua ya makundi kwani awali walishinda bao 2-1 dhidi ya Sierra Leone, timu nyingine ni Senegal, Algeria, Burkina Faso na Mali

Author: Bruce Amani