Samatta Atoa Matumaini kwa Watanzania Kuikabili Niger

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Ally Samatta amesema wamejipanga kuanza vyema kampeni ya kuwania tiketi ya kufuzu fainali za Afcon 2023 zitakazochezwa Ivory Coast.

Taifa Stars itaanza kampeni hiyo Jumamosi Juni 4 kwa kucheza ugenini dhidi ya Niger nchini Benin, na tayari imewashawasili Cotonou kwa ajili ya mchezo huo, utakaoanza majira ya saa moja kwa saa za Afrika Mashariki.

Samatta ambaye ni nahodha wa kikosi hicho amesema dhamira waliyoondoka nayo jijini Dar es salaam Alhamis ni kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo wakiamini kufanya.

“Mawazo yetu ni kuanza vizuri kampeni za AFCON 2023, kwa sababu ndio mchezo wetu wa kwanza, bahati mbaya tunaanzia ugenini, lakini upande mwingine ni bahati nzuri kwa sababu unapopata matokeo mazuri ugenini kwa kiasi fulani inakuongezea kujiamini katika kamepni nzima, kwa hiyo lengo ni kwenda kuanza vizuri.”

Baada ya mchezo wa kesho Jumamosi Juni 4, Stars itarejea nchini kucheza mchezo wa mzunguuko wa pili wa Kundi F dhidi ya Algeria utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Juni 08.

Author: Asifiwe Mbembela