Misri bila ya Salah yachapwa na Ethiopia mechi ya kufuzu AFCON 2023

Misri ilimkosa nahodha wake ambaye ni majeruhi Mohamed Salah wakati walipata kipigo cha 2 – 0 na Ethiopia jana katika mechi ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2023. Ethiopia walilazimika kucheza mechi hiyo mjini Lilongwe kwa sababu hawana viwanja vinavyokidhi viwango vya kimataifa.

Timu zote katika Kundi D ambazo ni Ethiopia, Malawi, Misri na Guinea, zimeshinda mechi moja na kupoteza moja kwa hiyo kila mmoja ana pointi tatu. Guinea ilipata ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Malawi mjini Conkary kupitia bao la Naby Keita.

Nigeria ilipata iliipiga Sierra Leone 2-1 katika Kundi A mjini Abuja. Guinea Bissau inaongoza kundi hilo kwa faida ya mabao kwa kuizaba Sao Tome e Principe 5-1. Kundi K, Afrika Kusini iliifungwa na Morocco 2 – 1. Cameroon waliwafunga Burundi 1 – 0 nchini Tanzania wakati Lesotho wakiwabana Cote d’Ivoire kwa sare tasa. Mali iliifunga Sudan Kusini 3 -1 katika Kundi G.

Author: Bruce Amani