Ndoto za Kenya kufuzu Afcon zazimwa na sare ya 1-1 na Misri jijini Nairobi

Matumaini finyu ya Kenya kujikatia tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika – AFCON mwaka ujao nchini Cameroon yamezikwa kabisa Alhamisi baada ya Harambee Stars kutoka sare ya 1 – 1na Misri.

Matokeo hayo yalimaanisha kuwa Misri walijiunga na Comoros katika kujikatia tiketi ya mashindano hayo ya Cameroon.

Stars ililazimika kucheza dakika 14 za mwisho na wachezaji 10 viwanjani baada ya Johnstone Omurwa kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kuzusha ugomvi na Ahmed Mostafa.

Kufuatia matokeo hayo ya Alhamisi, mechi za Jumatatu ambapo Kenya itacheza ugenini dhidi ya Togo na Misri itakuwa nyumbani dhidi ya Comoros haitakuwa na umuhimu.

Author: Bruce Amani