Stars Yaadhibiwa Kwa Mkapa 2-0 na Algeria

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imeangukia pua kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya taifa la Algeria katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika Afcon 2023 nchini Ivory Coast.

Ukiwa mchezo wa kwanza Stars Kucheza uwanja wa nyumbani ww Benjamin Mkapa, walijikuta wako nyuma kwa bao moja kunako dakika za mwisho za ungwe ya kwanza kupitia mpira wa kichwa wa Amir Selmane Ramy Bensebaïni dakika ya 45 ambapo bao lingine likifungwa na M. Amoura dakika ya 89.

Kwa matokeo hayo Algeria inafikisha pointi sita na kuendelea kuongozi kundi F kufuatia ushindi wa 2-0 kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Uganda Jijini Algiers Jumamosi.

Taifa Stars baada ya sare ya 1-1 ugenini na Niger sasa ni ya tatu. Niger baada ya sare ya 1-1 na Uganda leo Jijini Kampala inapanda nafasi ya pili na Uganda sasa inashika mkia.

Author: Asifiwe Mbembela