Ruvu Shooting yaibana Simba mkia na kulazimisha sare

Simba SC imetoshana nguvu na Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu nchini Tanzania, mtanange uliopigwa dimba la Taifa Jumapili.

Goli la Simba limefungwa na Shiza Ramadhan Kichuya akitumia vyema makosa ya walinzi wa Ruvu Shooting pamoja na kipa Mohammed Makaka ambaye alikuwa katika kiwango bora licha ya makosa hayo.

Upande wa Ruvu Shooting goli limetiwa kimiani na Fully Zulu Magaga likiwa ni la kusawazisha, ambapo Abdulahmann Mussa alikuwa kwenye kiwango bora sana.

Unakuwa mchezo wa 29 kwa Simba, alama moja waliyoipata inafikisha pointi 72 kwenye nafasi kwanza wakati Ruvu Shooting inafikisha pointi 40 lakini wataendelea kusalia nafasi ya 11 dhidi ya Biashara United ambayo nayo ina pointi hizo lakini wana tofauti za kufunga na kufungwa baada ya michezo yao 29.

Siku ya Jumamosi Simba itakuwa na kibarua kingine dhidi ya Mwadui Fc mchezo utachezewa nyasi za uwanja wa Taifa, Simba wakiwa wametoka kutoa sare hiyo watakutana na Mwadui ambayo imepigwa na Yanga dimba la CCM Kambarage.

Author: Bruce Amani