Tetesi za usajili Ulaya: Raul Jimenez kutua Real Madrid

Karibu katika taarifa mbalimbali zinazohusu tetesi za usajili barani Ulaya katika kipindi hiki ambacho duniani inatumia nguvu kubwa kukabiliana na virusi vya Corona, Amani Sports News inakuletea tetesi za usajili barani Ulaya siku ya leo Ijumaa, Aprili 3, 2020.

Klabu ya Liverpool imesimamisha mazungumzo yote ya kimkataba na wachezaji wapya mpaka pale ambapo janga la virusi vya Corona litakapomalizika, hiyo ina maanisha kuwa usajili wa straika wa RB Leipzig Timo Werner, 24, umesitishwa mpaka tamati ya COVID-19.

Straika wa Bournemouth Callum Wilson, 28, amesema hastahili kuhusishwa na vilabu vikubwa vya Ligi Kuu England kwa sababu msimu huu haukuwa mzuri kwake.

Mshambuliaji wa Gent na Canada Jonathan David, 20, amesema angependa kucheza ligi ya England kuliko ligi nyingine yoyote.

Fowadi wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, 30, na winga wa Manchester City Leroy Sane, 24, ni miongoni mwa wachezaji wanaoziumiza vichwa vilabu vyao juu ya mshakabali wa maisha yao ndani ya klabu hizo.

Raul Jimenez, 28, ameweka bayana kuwa hana kipengele cha mkataba ambacho kina mlazimisha kutoondoka Wolves kama itatokea klabu yoyote yupo tayari kuondoka, Manchester United, Real Madrid na Chelsea zote zimeonyesha nia ya kuhitaji saini ya fowadi huyo.

Kiungo wa Kihispania Dani Ceballos, 23, amewekwa kwenye orodha ya wachezaji ambao huenda wakauzwa moja kwa moja na klabu ya Real Madrid, ambapo Arsenal imekuwa ikihaha kumnasa staa huyo.

Manchester United wamehairisha kusajili beki wa kushoto baada ya kuibuka kwa kinda Brandon Williams, 19, anayefanya vizuri na kuweka ushindani dhidi ya Luke Shaw.

Manchester United huenda wakatuma dau la £70 kwenda kwa kiungo wa Atletico Madrid Saul Niguez, 25, ambapo kiungo huyo amekuwa akihusishwa kwa siku za karibuni.

Staa wa Aston Villa Jack Grealish, 24, ameambiwa kuwa kuna uwezekano mdogo wa yeye kujiunga na Manchester United katika dirisha kubwa la usajili.

Aston Villa wanahusishwa na kiungo wa Marseille Maxime Lopez, 22.

Kama ilivyo kawaida kwa mshambuliaji wa Tottenham na Korea Kusini Son Heung-min, 27, kuhudhuria mafunzo ya kijeshi, basi msimu huu amepanga kwenda kumalizia kutoa huduma ya kijeshi katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama. Son amekuwa na utaratibu huo kama kanuni za nchi hiyo.

Kiungo mshambuliaji wa Manchester City Kevin de Bruyne, 28, ameonya kutokea kwa majeruhi kwa wachezaji endapo ligi itarejea bila kuwepo kwa maandalizi kwa wachezaji.

Author: Bruce Amani