Yanga yamaliza ligi kwa machozi kwa kulimwa na Azam

Azam FC imeibuka na ushindi dhidi ya Yanga katika mchezo wa kufungia pazia la Ligi Kuu Tanzania bara kwa ushindi mnono wa goli 2-0 na kuwaachia simanzi Yanga katika mtanange uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga na Azam zikiwa hazina cha kupoteza msimu huu baada ya kushindwa kutwaa taji la TPL wakishuhudia likienda kwa Simba, waliingia kwenye mchezo kwa hali finyu huko kila timu ikicheza katika upande wake zaidi.

Muda ulivyokuwa unasonga ndivyo ushindani ulivyoongezeka na kupelekea timu kuanza kushambuliana kwa kasi katika vipindi tofauti, kuna wakati Azam ilitawala hali kadhalika Yanga pia.

Baada ya piga nikupige Azam walifanikiwa kupata goli la kuongoza dakika ya 45 kipindi cha kwanza kupitia kwa Daniel Amouh na bao la pili limefungwa na Mudathir Yahya dakika ya 50 na kukamilisha furaha ya kumaliza ligi Kuu kwa ushindi.

Timu zote mbili zilikuwa zinatafuta heshima kwenye uwanja wa Taifa leo ikiwa ni mchezo wa mwisho kwa msimu huu.

Ushindi wa leo kwa Azam unatafasiriwa kama ni kisasi kwa Yanga mara baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza Yanga kushinda kwa goli 1-0, goli la Mrisho Ngassa.

Baada ya mchezo huo Afisa Habari wa Azam Jaffar Idd Maganga amesem nguvu zao wanaziamishia kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) watakapo papatua dhidi ya Wanapaluengo Lipuli FC kwenye uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi.

Azam atacheza na Lipuli Juni Mosi, 2019 katika kusaka timu ya pili itakayoiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika – CAF.

Author: Bruce Amani