Ambokile mchezaji bora wa Septemba

Mshambuliaji wa timu ya Mbeya City ya mkoani Mbeya Eliud Ambokile, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Septemba wa Ligi kuu Tanzania, baada ya kuzoa kura nyingi na kuwashinda wachezaji Ibrahim Ajib wa Young Africans na Stamili Mbonde wa Mtibwa Sugar.

Mwezi September ulikua mwezi bora kwa Ambokile kwa kufunga magoli manne akiisaidia timu yake kupanda kileleni katika msimamo wa ligi kuu huku pia akiwa kinara wa kufunga magoli katika ligi hii kwa kufumania nyavu mara sita.

Ambokile anakuwa mchezaji bora wa pili wa mwezi katika msimu wa 2018-2019, baada ya mshambuliaji wa mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu wekundu wa Msimbazi Simba Meddie Kagere raia wa Rwanda

Kwa ushindi huo, bodi ya ligi itamzawadia tuzo na shilingi milioni moja pamoja na kisimbusi cha Azam.

Author: Bruce Amani

AmbokileMbeya City