Bach akanusha kuwa IOC ilisita kuchelewesha michezo ya Olimpiki

Rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach amepinga madai kuwa kamati hiyo ilisita kutoa uamuzi juu ya kuahirishwa kwa michezo ya Olimpiki ya majira ya joto kutokana na janga la virusi vya Corona.

Bach ameliambia gazeti la Ujerumani la Welt am Sonntag kuwa anaelewa kwanini watu walikuwa na fikra hiyo.

Mnamo Machi 24, kamati hiyo ya IOC ilitangaza kuwa itaifuta michezo ya Olimpiki msimu huu wa majira ya joto kufuatia kuenea kwa virusi vya Corona na baadaye ikaamua badala yake kuahirisha michezo hiyo kwa karibu mwaka mmoja.

Bach amesisitiza kuwa kuifuta michezo hiyo haikuwa chaguo la kamati hiyo.

Ameongeza kuwa uamuzi wa kuifuta kabisa michezo hiyo ya Olimpiki haukuungwa mkono na wawakilishi wa wanariadha kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Author: Bruce Amani