Mauritania yapewa kipigo mikononi mwa Mali

Wageni Mauritania wamekaribishwa vibaya kwenye michuano ya Kimataifa Afrika AFCON baada ya kukubali kipigo kikubwa cha mashindano mpaka sasa cha goli 4-1  dhidi ya Mali katika Kundi E.

Timu zote zikiwa zinatokea ukanda wa Afrika Magharibi zilianza mchezo kwa kasi lakini ukosefu wa uzoefu ulionekana changamoto kwa Mauritania kitu kilichowaponza zaidi.

Ushindi wa Mali ulipitia magoli yaliyofungwa katika dakika za mwanzo za kipindi cha kwanza kupitia kwa Abdoulaye Diaby na Moussa Marega, na Adama Traore goli (2) ya kabla ya Mauritania kupata goli la kufutia machozi kupitia kwa Hacen Al Ide.

Matokeo hayo yanaifanya Mali kuongoza kundi E kwa alama tatu wakati Tunisia na Angola nafasi ya pili na ya tatu baada ya mchezo wao kutoa sare na wageni Mauritania ya mwisho kwa kutokuwa na alama hata moja.

Haya ni mashindano ya kwanza kwa Mauritania kushiriki huku kikiwa kipigo kikubwa zaidi kwao.

Author: Bruce Amani