Mbappe Aipiku Rekodi ya Cavani PSG

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe ameipiku rekodi ya mfungaji bora katika kikosi cha matajiri wa Paris, Paris St-Germain baada ya kufunga bao moja kwenye ushindi wa goli 4-2 dhidi ya Nantes mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa – Ligue 1.

Bao moja hilo lilifikisha 201 idadi ya mabao yake na kuipiku rekodi ya fowadi wa zamani wa klabu hiyo Edinson Cavani ambaye alikuwa anashikilia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote kwa bao 200.

Mabao mengine ya PSG yamefungwa na Lionel Messi, Jaouen Hadjam akijifunga, pamoja na bao la Danilo ambaye goli lake lilikuwa la tatu.

Mabao ya Nantes ambao msimu huu wanaendelea kuonyesha kiwango maridhawa yamefungwa na Ludovic Blas na Ignatius Ganago wakimshinda ujanja mlinda mlango Gianluigi Donnarumma.

Author: Asifiwe Mbembela