Mbappe Aweka Rekodi ya Kibabe Ufaransa

Kylian Mbappe amehusika kwenye magoli sita kwenye mchezo wa Kombe la Ufaransa baada ya kufunga mabao matano na kutoa assisti kwa bao moja kwenye mtanange dhidi ya timu ya daraja la chini ya Pays de Cassel.

Ushindi wa PSG unaifanya ifuzu kucheza robo fainali ya Kombe hilo wakichuchumilia taji la 14, huku kikosi cha matajiri hao kikilazimika kusubiri mpaka dakika 29 za mchezo kufunga goli la kwanza.

Mbali na Mbappe aliyefunga mabao matano, wachezaji wengine waliofunga ni staa wa Brazil Neymar Jr, Carlos Soler.

Magoli hayo matano kwa Kylian Mbappe ambaye mara ya mwisho kufunga magoli mengi hivi karibuni ilikuwa dhidi ya Argentina kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Dunia Qatar yanamfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga idadi kama hiyo kwenye mchezo mmoja kwa PSG.

Author: Asifiwe Mbembela