Messi Arudi na Magoli PSG

Nyota wa kimataifa wa Argentina taifa bingwa la Kombe la Dunia Qatar Lionel Messi amerejea uwanjani na goli na kuisaidia klabu yake ya Paris St-Germain kushinda bao 2-0 dhidi ya Angers mchezo wa Ligi Kuu nchini Ufaransa Ligue 1.

Messi, 35, akiwa na ruhusa maalumu hakuweza kurejea kambini ngazi ya klabu kama wenzake baada ya kufunga bao saba na kushinda mchezo wa fainali kwa Ufaransa.

Hugo Ekitike alifunga bao la kwanza kabla ya Messi kutupia kunyavu goli la pili.

PSG baada ya ushindi huo wanakuwa kileleni kwa pointi sita zaidi ya Lens waliopo nafasi ya pili ambao wamesare 2-2 na Strasbourg.

Author: Bruce Amani