Messi Aipa PSG Ushindi kwa Toulouse

Paris St Germain imetokea nyuma ya goli moja bila na kushinda bao 2-1 dhidi ya Toulouse katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ufaransa Ligue 1.

Wakiwa katikati ya msimamo wa Ligue 1, Toulouse waliweza kutangulia kupata bao kupitia mpira wa kutengwa wa kiungo wa Kiholanzi Van den Boomen kabla ya kuanza kushindwa kuhimili vishindo vya PSG.

Achraf Hakimi alifunga bao la kwanza kwa PSG kisha mshindi wa Kombe la Dunia Qatar 2022 Lionel Messi akafunga bao la ushindi kwa PSG.

Matokeo hayo yanaifanya kukwea mpaka nafasi ya kwanza wakiwa na alama 54 alama nane zaidi ya Marseille nafasi ya pili.

Author: Asifiwe Mbembela