Ni Algeria au Ivory Coast robo fainali Afcon 2019?

Leo Julai 11, Algeria wanaikabili Ivory Coast kwenye mashindano ya Afcon 2019 nchini Misri, mtanange wa hatua ya robo fainali utachezwa katika dimba la Suez kuanza majira ya 1 usiku.

Huu unakuwa mchezo wa nane kwa timu hizo kukutana kwenye michuano ya Afcon huku rekodi zikiibeba zaidi Ivory Coast ambayo imeshinda tatu wakati Algeria imeshinda mara mbili tu na sare mbili pia.

Mwaka 1968, 1992 na 2015 Ivory Coast iliibuka na ushindi wakati mwaka 1990 na 2010 Algeria iliishinda na sare mbili 1988 na 2013.

Asilimia 95 ya kikosi cha Ivory Coast kilichocheza mchezo wa mwisho dhidi ya Algeria wachezaji watano tu ndio wapo kwenye kikosi cha sasa, Gradel, Wilfred Bony ni miongoni mwa walikuwepo kikosini.

Algeria iliitoa Guinea hatua ya 16 bora kwa ushindi wa goli 3-0 wakati Ivory Coast ikishinda 1-0 dhidi ya Mali.

Author: Bruce Amani