Simba yatua Msumbiji kuivaa Songo Ligi ya Mabingwa Afrika

Simba imewasili Msumbiji salama kuwavaa wenyeji wao UD Songo ya nchini humo mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua za awali mtanange utakaopigwa Jumamosi kuanzia saa 11 jioni masaa ya Afrika Mashariki.
Simba ambayo ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wameshatia timu nchini Msumbuji kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa kesho dhidi ya UD do Songo.
Simba ilikwea pipa leo asubuhi kutoka Bongo kwa ndege binafsi ili kukwepa usumbufu na wanatarajia kurejea kesho baada ya kumaliza mchezo huo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.
Kuelekea mchezo huo Simba itawako wachezaji saba ambao ni :- Said Ndemla, Yusuf Mlipili, Kennedy Juma, Aishi Manula, Wilker da Silver, Ibrahim Ajib, Haruna Shamte na Miraj Athuman.
Mbali na mchezo huo wa Simba, Tanzania itakuwa ikizitazama timu zao ambazo wikendi hii zitakuwa uwanja.
Siku ya Jumamosi(kesho) Yanga itacheza na Township Rollers ya Botswana, Kmc dhidi ya AS Kigali na siku ya Jumapili Azam watakuwa ugenini nchini Ethiopia.

Author: Bruce Amani