Bayern wanyimwa ubingwa Bundesliga na Mainz, wachapwa 2-1

Bayern Munich watasubiri kuthibitishwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu nchini Ujerumani Bundesliga kwa mara ya 9 mfululizo baada ya kukutana na kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa Mainz.

Vinara hao wa Bundesliga walikuwa wanahitaji ushindi mmoja tu kutoka kwenye mechi tatu zilizosalia kukabidhiwa taji la Bundesliga kwa mara nyingine tena.

Hata hivyo, kwenye mechi hiyo walianza kupigwa mapema kabisa kupitia kwa Jonathan Burkardt, 18, kabla ya Robin Quaison kuongeza bao la pili.

Bao la kufutia machozi kwa Bayern Munich limefungwa na mshambuliaji Robert Lewandowski aliyekuwa majeruhi katika dakika ya 90.

Mainz wanakamata nafasi ya 12 baada ya matokeo hayo.

Author: Bruce Amani